IQNA

Maonyesho ya picha za Ashuraa kufanyika Uturuki

14:52 - November 21, 2010
Habari ID: 2034980
Katika kukaribia mwezi wa Muharram ambao ni mwezi wa damu na shahada, maonyesho ya picha za Ashuraa yamepangwa kufanyika mjini Istanbul Uturuki kuanzia tarehe 22 hadi 30 Novemba.
Kwa mujibu wa tovuti ya Zainabiyya ambayo ni ya Mashia wa Uturuki, maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na jumuiya ya CAFERİDER kwa ushirikiano wa Meya wa Istanbul yatafanyika katika kituo cha utamaduni cha Bülent Ecevit kilichoko upande wa Asia wa mji huo. Maonyesho mengine kama hayo yamepangwa kufanyika tokea tarehe Mosi hadi 15 Disemba katika kituo ha utamaduni cha Cem Karaca katika upande wa Ulaya.
Istanbul ndio mji mkubwa zaidi wa Uturuki na kituo chake muhimu cha kiutamaduni na kiuchumi. Huo ni mji wa pekee mkubwa ulioko katika mabara mawili ya Ulaya na Asia. 698639
captcha