Kituo cha habari cha American Consumer News kimeripoti kuwa kitabu hicho cha Qur'ani ya sauti kimesomwa na Alec Sand kwa masaa 14 na dakika 40. Kitabu hicho kimewekwa katika sehemu ya vitabu vya dini na masuala ya kiroho ya mtandao wa Audible.com.
Katika kuarifisha kitabu hicho, mtandao huo umeandika kuwa: "Qur'ani Tukufu ni moja ya vitabu vyenye taathira kubwa vya mbinguni. Mbali na hayo Qur'ani ni kinara katika medani ya fasihi na kiliteremshwa na Malaika Jibrail kwa Mtume wa Uislamu miaka 1400 iliyopita. Kitabu hicho kinatambuliwa na Waislamu wote duniani kuwa ni neno la Mwenyezi Mungu linalokusanya masuala yote ya maisha.
Kituo cha intaneti cha Audible.com kiko chini ya mtandao mashuhuri wa Amazon.com, ambacho ndio muuzaji mkubwa zaidi wa vitabu, majarida na vipindi vya redio na televisheni katika mtandao wa intaneti. 700492