Hayo yamesemwa na Mkuu wa Taasisi ya Jihad ya Vyuo Vikuu nchini Iran Bw. Mohammad Yadegari. Akizungmza na IQNA, amesema kuwa, ‘kwa maoni yangu mashindano kama haya yanaweza kuwa na nafasi muhimu ya kustawisha mabadilishano ya mawazo baina ya wanachuo kutoka nchi mbali mbali jambo ambalo bila shaka litakuwa na matunda mema’.
Yadegar amesema kuwa maadui wanatumia kila mbinu kutoa taswira potofu kuhusu Jamhuri ya Kiislamu duniani na kwa kuzingatia hilo, ‘mashindano ya Kimataifa ya Qurani Tukufu nchini Iran yanaweza kuwa na nafasi muhimu kuvunja njama hizo za maadui’.
Mashindano ya Tatu wa Kimataifa ya Qurani Tukufu ya Wanachuo Waislamu yatafanyika Januari 19-22 mwaka 2011 katika mji mtakatifu wa Mashhad.
699670