IQNA

Hijabu yaruhusiwa katika jimbo la Saxony nchini Ujerumani

16:03 - November 28, 2010
Habari ID: 2038998
Wizara ya Elimu ya Jimbo la Saxony nchini Ujerumani imesema kuwa wanafunzi wa kike wa Kiislamu katika jimbo hilo wako huru kuvaa vazi la Kiislamu la hijabu wanapokuwa shuleni.
Hata hivyo viongozi wa elimu wa jimbo hilo wamesisitiza kwamba hawatawaruhusu wanafunzi hao kuvaa vazi linalofunika kabisa nyuso zao, mashuhuri kwa jiba la burqa na kwamba watakaoruhusiwa kushiriki katika ratiba za masomo katika mazingira ya shule ni wale tu watakaovaa hijabu ya kawaida ya Kiislamu inayositiri miili na nywele zao. Katika hatua nyingine inayofanana na hiyo, daktari mmoja wa kike katika jimbo la Waechtersbach amelazimishwa na Jumuiya ya Madkari ya Ujerumani kuwahudumia kitiba wanawake wa Kiislamu wanaovaa hijabu baada ya daktari huyo kukataa kufanya hivyo kwa muda. Daktari huyo ameonywa na kutakiwa awahudumie wanawake wa Kiislamu baada ya wao kuchukua hatua ya kuilalamikia jumuiya hiyo kuhusiana na kitendo cha daktari huyo cha kukataa kuwahudumia kwa kisingizio cha wao kuvaa hijabu. 702223
captcha