Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maudhui kuu ya kongamano hilo litakalofanyika Zambia ni "Falsafa ya Kuomboleza Mwezi wa Muharram'.
Ali Bakhtiari Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Zambia anatazamiwa kutoa hotuba katika kikao hicho.
Zambia ni nchi ya kusini mwa Afrika na Waislamu nchini humo wanakadiriwa kuwa karibu asilimia tano ya watu wote millioni 11.26 nchini humo.
705539