IQNA

Madaktari wa OIC waanza shughuli zao Ghaza

15:23 - December 05, 2010
Habari ID: 2042140
Ujumbe wa madaktari kutoka Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC umewasili katika Ukanda wa Ghaza katika awamu ya kwanza ya misaada ya kitiba kwa Wapalestina waliojeruhiwa katika hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ardhi hiyo ya Palestina.
Kwa mujibu wa jarida la Middle East Monitor, ujumbe huo umetumwa kufuatia ushirikiano wa OIC na Jumuiya ya Misaada ya Salama pamoja na Hospitali ya Baslam huko Ghaza.
Mtaalamu wa upasuaji kutoka Jordan Daktari Mohammad el-Abady amesema ameshangazwa na hali mbaya ya Wapalestina wanaohitajia matibabu ya dharura.
Itakumbukwa kuwa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilitumia mabomu ya sumu yaliyopigwa marufuku katika hujuma yake ya kinyama ya wiki tatu dhidi ya Ukanda wa Ghaza mwaka 2008/2009. Natija ya hujuma hiyo ni majeraha ambayo madaktari wanasema hawajawahi kuona mfano wake. 706158

captcha