Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Al Hafiyian ambaye pia alikuwa mhadhiri katika Taasisi ya Sharia ya Kiislamu ya Tunisia aliaga dunia Jumapili Disemba 5 kufuatia maradhi ya moyo.
Karii huyo mashuhuri wa Tunisia alipokuwa ndani ya ndege akirejea kutoka safari ya hija wiki mbili zilizopita alipata matatizo ya moyo jambo lililoilazimisha ndege aliyokuwemo kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Cairo na kukimbizwa hospitalini. Alibakia hospitalini hapo hadi alipoaga dunia.
Shughuli zingine za marhum Abdul Rahman Al Hafiyian zilikuwa ni pamoja na khatibu wa sala ya Ijumaa, mwalimu katika Jumuiya ya Qur'ani ya Tunisia, Mkurugenzi wa Masomo ya Qur'ani katika 'Radio Zaituna' ya Tunisia.
Ustadh al Hafiyian ambaye alikuwa na shahada ya utaalamu wa kiraa ya Qur'an ameandika vitabu kadhaa kuhusu elimu ya tajwidi. 707793