Kwa mujibu wa tovuti ya Liverpool-Shia, maombolezo hayo ambayo yataendelea hadi disemba 17 yatakuwa yakifanyika kila siku kuanzia saa moja hadi tatu na nusu usiku kwa wakati wa Uingereza. Kusimamishwa swala za jamaa, hotuba za Hujjatul Islam wal Muslimin Waidhi na makumbusho ya kuuawa shahidi Imam Hussein (as) ni miongoni mwa ratiba zitakazotekelezwa katika maombolezo hayo ya Manchester.
Kwa mnasaba huo, Kituo cha Tauhidi cha Liverpool cha Uingereza kitakuwa kikitekeleza ratiba tofauti za maombolezo ya Imam Hussein (as) katika kituo hicho kuanzia tarehe 11 hadi 16 Disemba.
Katika siku ya Ashura tarehe 16 Disemba, kituo hicho kitatekeleza ratiba maalumu kwa jina la 'Adhuhuri ya Ashura' kuanzia saa tano hadi saa saba ili kukumbuka umuhimu wa kuuawa shihidi Imam Hussein (as) katika siku hiyo. 708091