IQNA

Mashindano ya Qur'ani yazingatie tafsiri ya kitabu hicho

18:48 - December 08, 2010
Habari ID: 2044793
Wito umetolewa wa kutaka tafsiri ya Qur'ani izingatiwe zaidi kuliko kiraa katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanachuo wa Kiislamu ambayo hufanyika Iran kila mwaka.
Hujjatul Islam Hamid Mohammadi Naibu Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu anayehusika na masuala ya Qur'ani amesema kuzingatiwa zaidi tafsiri ya Qur'ani kutainua kiwango cha mashindano hayo.
Amesisitiza kuwa vyanzo vya tafsiri vinapaswa kuchaguliwa miongoni mwa tafsiri zinazokubaliwa kwa pamoja na madhehebu ya Shia na Suni.
Amesema kuwa mashindano hayo ni fursa nzuri ya kuarifisha utambulisho wa Qur'ani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qurani ya Wanachuo Waislamu yatafanyika katika mji wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran mwezi ujao wa Januari 9-11.
706686
captcha