Huku ikisisitiza udharura wa kulindwa Quds Tukufu na maeneo matakatifu, Kamisheni ya Kiislamu na Kikristo ya Kulinda Quds na Maeneo Matakatifu imetahadharisha kwamba Wazayuni wanapanga njama ya kubomoa sehemu ya kaskazini ya Msikiti wa al-Aqsa na maeneo mengine yanayouzunguka msikiti huo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Palestine info, Hassan Khatir, Mkuu wa kamisheni iliyotajwa amefichua habari kwamba Wazayuni hivi sasa wanasubiri kushuhudia kubomoka kwa msikiti huo kutokana na uchimbaji ambao wamekuwa wakiufanya katika msikiti huo.
Hassan Khatir amesema kuwa kulindwa msikiti huo ni jukumu la kila Mwislamu na ametaka Jumuiya Nchi za Kiislamu na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ziunde kamati ya wahandisi na wataalamu mashuhuri wa masuala ya usanifu majengo watakaotembelea Msikiti wa al-Aqsa ili kuufanyia uchunguzi zaidi. 708326