Mkutano huo utasimamiwa na Jumuiya ya Utamaduni ya Lugha ya Waislamu wa Uswisi ikishirikiana na Taasisi ya Utamaduni ya Waislamu wa nchi hiyo kwa lengo la kuwakutanisha pamoja Waislamu wapya wa miji mbalimbali ya nchi hiyo.
Miongoni mwa ratiba za mkutano huo ni kutambuana, kufanya mazungumzo kuhusu sababu za kusilimu wafuasi wa dini mbalimbali na kuchunguza njia za kuamiliana familia za Kiislamu na watoto wao ambao bado hawajakubali dini ya Kiislamu.
Maonyesho ya vitabu na turathi za kiutamaduni za Kiislamu pia yatafanyika wakati wa mkutano huo. 709160