IQNA

Ushia ni madhehebu ya ushirikiano na wafuasi wa dini tofauti

18:04 - December 11, 2010
Habari ID: 2046077
Boris Boillon, balozi wa Ufaransa nchini Iraq amesema kuwa Ushia ni madhehebu ya usamehevu, ushirikiano na mawasiliano mazuri na wafuasi wa dini tofauti.
Balozi huyo amesema kuwa watu wa Ufaransa wanauheshimu Ushia kwa sababu ni madhehebu ya usamehevu, ushirikiano na mawasiliano mazuri na wafuasi wa dini nyinginezo kinyume na inavyodaiwa na baadhi ya watu. Ameongeza kuwa kuna baadhi ya watu wanaojaribu kudhihirisha sura potofu na isiyo sahihi kuhusiana na Uislamu na hasa madhehebu ya Shia.
Balozi Boillon ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na mafisa wa serikali katika mji mtakatifu wa Karbala na kuongeza kuwa mji huo ni moyo hai wa madhehebu ya Shia. 710628
captcha