Hayo yamesema na Abdulhadi al Salih mbunge wa zamani Kuwait ambaye pia ni mwanaharakati wa kisiasa. Gazeti la Al Anbaa la Kuwait limemnukulu Abdulhadi al Salih akiongeza kuwa: "Mtu wa kwanza kulia kwa ajili ya Imam Hussein AS alikuwa Mtume Mtukufu Muhammad SAW na kuna hadithi nyingi kuhusu suala hili".
Ameongeza kuwa: "Mwamko na harakati ya Imam Hussein AS si suala ambalo lilisahaulika na kuisha zaidi ya miaka 1400 iliyopita baada ya kuuawa shahidi mtukufu huyo, bali mapambano ya Abu Abdillah Hussein AS yatabakia hai hadi Siku ya Kiyama. Harakati ya mapambano ya Bwana wa Mashahidi (AS) ilikuwa kwa ajili ya kufanya marekebisho katika umma wa kuamrisha mema na kukataza mabaya. Harakati hiyo ni ya nyakati na zama zote".
Salih ameongeza kuwa: "Imam Hussein AS ni shakhsia ambaye ni kigezo kinachostahiki kubakia katika zama zote. Kuhusiana na hili Mtume SAW alisema: "Hussein ametokana nami na mimi nimetokana na Hussein, Mwenyezi Mungu anampenda kila anayempenda Hussein".
Mwanasiasa huyo wa Kuwait amesema kuwa hadithi hii ya Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW inasisitiza juu ya nafasi kubwa na daraja ya juu ya Imam Hussein AS kwa Mtume SAW.
710475