Kwa mujibu wa gazeti la al-Bilaad, warsha hiyo inadhaminiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu na Uhubiri ya Saudi Arabia kwa ushirikiano wa Idara Kuu ya Jumuiya za Masuala ya Kheri na Hifdhi ya Qur'ani ya nchi hiyo.
Mkuu wa Idara hiyo Uthman bin Muhammad as-Swidiqi amesema kuhusiana na suala hilo kwamba warsha hiyo itafanyika kwa lengo la kuwasilisha maana halisi ya Qur'ani, kuimarisha uhusiano kati ya wanachuo wanaosoma masomo ya Qur'ani, kutekeleza mafundisho ya Qur'ani kupitia masomo katika ngazi mbalimbali na kujipamba kwa maadili ya Qur'ani. 711738