Mashindano hayo yatafanyika katika makao makuu ya Taasisi ya Kiitikadi-Kisiasa ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Tehran.
Mashindano hayo yatakuwa na vitengo vya kuhifadhi juzuu 6, juzuu 18 na Qur'ani kamili ambapo washiriki kutoka nchi zote mbili watashiriki katika kila kitengo.
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia linatazamiwa kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ya majeshi ya nchi za Kiislamu ambayo yataandaliwa na Saudi Arabia.
Mashindano ya Qur'ani ya majeshi ya nchi za Kiislamu yalianzishwa na Iran mwaka 1993 na yamefanyika mara tatu nchini Iran, mara tatu nchini Saudi Arabia na mara mbili nchini Pakistan. Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lilichukua nafasi za kwanza katika aghalabu ya mashindano hayo.
711087