IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Ras al-Khaimah Imarati

12:44 - December 18, 2010
Habari ID: 2048583
Awamu ya 11 ya Mashindano ya Qur'ani ya Kitaifa ya Ras al-Khaima katika Umoja wa Falme za Kiarabu yamepangwa kuanza Februari 11.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, waandalizi wa mashindano hayo wamesema yatakuwa na washiriki 175 katika viwango vya kuhifadhi Qur'ani Tukufu ambapo kutakuwa na makundi mawili ya wanaume na wanawake.
Umar ibn Abdulaziz al Qasimi wa kamati andalizi ambaye pia ni mwanachama wa Taasisi ya Sayansi za Qur'ani ya Ras al Khaima amesema, “wanafunzi kutoka vituo vya kufunza Qur'ani watashiriki katika mashindano hayo ambayo yatakuwa na washindano 78 wa kike na 97 wa kiume”.
Ameongeza kuwa washiriki wa mashindano ya hifdhi watakuwa wa kitaifa huku viwango vingine vikishirikisha wakaazi wa Ras al Khaima pekee.
Al Qasimi amesema wanaoandaa mashindano ya mwaka huu wanajitahidi kuhakikisha kuwa yamefana na malengo yaliyoainishwa yanafikiwa.
713311
captcha