IQNA

Kitabu cha "Misamiati ya Qur'ani katika Zama Mbalimbali" chachapishwa Misri

8:36 - December 19, 2010
Habari ID: 2049308
Kitabu chenye anwani ya "Misamiati ya Qur'ani katika Zama Mbalimbali" kimechapishwa na Taasisi ya Uchapishaji ya Dar-al-Hilal mjini Cairo nchini Misri.
Kwa mujibu wa gazeti Al Yawm al Sabi, kitabu hicho kimeandikwa na Muhammad Dawoud mtafiti wa Qur'ani Misri.
Siri za kudumu na kutoweza kubadilika Qur'ani Tukufu katika karne 14 zilizopita ni kati ya mada muhimu za kitabu hicho.
"Misamiati ya Qur'ani Tukufu ni ya kudumu milele na inaweza kukabiliana na changamoto zozote" imeandikwa katika kitabu hicho.
Muhammad Dawoud amesisitiza kuwa katika mitazamo ya mofolojia, sintaksi na semantiki, Qur'ani Tukufu imeipa lugha ya Kiarabu uthabiti na kuifanya iwe ya kimuujiza.
Kitabu cha "Misamiati ya Qur'ani katika Zama Mbalimbali" kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu na ni kati ya vitabu vya hivi karibuni vilivyochapishwa na taasisi hiyo kuhusu Qur'ani.
captcha