Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Rasd, Sheikh al Habil ameongeza kuwa, 'lengo la maadui katika kutekeleza hujuma za kigaidi na kulenga waombolezaji wa Imam Hussein (sa) ni kuvuruga umoja wa umma wa Kiislamu na kuzusha fitina za kimadhehebu'.
Ameongeza kuwa, 'baada ya maadui kutambua kuwa dini tukufu ya Kiislamu inaenea kwa kasi kote duniani, sasa wanatekeeleza njama za kuleta hitilafu miongoni mwa Waislamu'.
Mwanazuoni huyo wa Kiislamu kutoka Saudi Arabia ametoa wito kwa umma wa Kiislamu kushikamana na umoja wa Kiislamu ili kuweza kuvunja njama za maadui za kuibia hitilafu za kimadhehebu. Sheikh al Habil pia ametoa wito kwa vijana wa Kishia nchini Saudia kushikamana na akhlaqi pamoja na thamani za juu za Kiislamu ambazo Imam Hussein (as) aliuawa shahidi kwa ajili ya kuzitetea na kuzilinda.
Sheikh Abdulkarim al Habil ni kati ya maulamaa wa ngazi za juu wa Kishia nchini Saudi Arabia. Yeye ni mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na vilevile Imamu wa Ijumaa katika mji Tarut mkoani Qatif. 714066