Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran zimearifu kuwa, Katibu Mkuu wa OIC Ekmeleddin Ihsanoglu amempongeza Salehi kwenye mazungumzo yao ya jana kupitia njia ya simu na kueleza matumaini kuwa, uhusiano kati ya Tehran na OIC utaendelea kuimarika.
Kwa upande wake Salehi amemshukuru Ihsanoglu kwa mawasiliano yake na kuelezea matumaini yake kuwa ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu utazidi kuimarika.
Jumatatu iliyopita, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran alimteua Ali Akbar Salehi kukaimu Wizara ya Mashauri ya Kigeni kuziba pengo lililoachwa na Manouchehr Mottaki ambaye amekuwa katika wadhifa huo tokea mwaka wa 2005.
713907