IQNA

Chuo cha kwanza cha Uchumi wa Kiislamu kuanzishwa Imarati

14:51 - December 19, 2010
Habari ID: 2049789
Chuo cha kwanza cha Uchumi wa Kiislamu na Maadili ya Kiutaalamu katika Mashariki ya Kati kitaanzishwa hivi karibuni huko Abu Dhabi mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la al-Bayaan lengo la kuanzishwa chuo hicho ni kunyanyua kiwango cha uelewa kuhusiana na umuhimu wa shughuli za biashara kwa msingi wa maadili na kusaidia taasisi tofauti kuimarisha utamaduni wa kuzingatia maadili katika jamii.
Chuo hicho kitazisaidia taasisi hizo kuendesha shughuli zao kwa msingi wa viwango vya juu zaidi vya kitaalamu na kusambaza tafiti tofauti kuhusiana na mbinu za kufanya kazi na biashara kwa msingi wa uchumi wa Kiislamu.
Akizungumzia suala hilo, Jauan Suheil al-Khalili Mkuu wa Bodi ya Idara ya Benki ya Kiislamu ya Abu Dhabi amesema kuwa benki hiyo imeazimia kutoa huduma za uwekezaji wa Kiislamu katika eneo na wakati huohuo kuonyesha maadili bora zaidi ya Kiislamu katika utoaji wa hudumu hizo. 714380
captcha