Akizungumzia suala hilo, Ridhwa Mulhis mkurugenzi wa idhaa hiyo amesema kwamba redio hiyo imefanikiwa kurusha tena hewani vipindi vyake kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na watu wanaojali pamoja na wapenzi wa idhaa hiyo. Amemshukuru gavana wa Nablos, Waziri wa Wakfu wa Palestina, Waziri wa Mawasiliano, Naibu Waziri wa Habari, Meya wa Nablos, Jumuiya ya Waandishi, taasisi za uhubiri na upashaji habari za Palestina, wasomi na wanafikra wa Palestina kutokana na juhudi hizo.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa idhaa hiyo imekuwa ikiheshimu kikamilifu sheria za uandishi na upashaji habari katika kipindi chote cha miaka 13 ya shughuli zake.
Wakati huohuo Hamid al-Baitawi, Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Palestina ambaye pia ni mbunge wa eneo hilo amekosoa vikali hatua ya ofisi ya mwendesha mashtaka wa Palestina ya kufunga idhaa hiyo na kusema kuwa hiyo ni sehemu ya ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina dhidi ya shughuli za Kiislamu katika Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. 714545