Kwa mujibu wa shirika la habari la Malaysia, Baharom amedai kwamba uamuzi huo umechukuliwa kwa shabaha ya kulinda nidhamu ya nchi hiyo ambayo wengi wa raia wake ni wafuasi wa madhebeu ya Suni. Ameitaka serikali na taasisi za kidini za nchi hiyo kufanya juhudi kubwa ili kuzuia kuenea Ushia katika nchi hiyo.
Mwishoni mwa wiki iliyopita askari usalama wa Malaysia waliwatia nguvuni Mashia 200 karibu na mji wa Kuala Lumpur kwa kisingizio cha kuhubiri Ushia nchini humo.
Madai ya uongo yamekuwa yakitolewa na viongozi wa serikali na duru nyinginezo zilizo na chuki dhidi ya madhehebu hii ya Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) au kwa jina jingine Ahlul Beit (as), yakiwemo yale yanayodai kuwa madhebeu hii inawashajiisha wafuasi wake kuwaua wafuasi wa dini nyinginezo, katika hali ambayo inafahamika vyema kwamba fikra hii ni ya Mawahabi na wala sio Mashia. 715984