Mashindano hayo yamesimamiwa na shule ya Zahratul Madain ya Palestina ikishirikiana na Idara ya Elimu ya mkoa wa Jericho na yamewashirikisha wanafunzi wa darasa la kwanza hadi nne.
Waamuzi wa mashindano hayo Aida al Sharbani, Aisha Maharima na Suha al Sibasi walitangaza washindi katika nyanja mbalimbali za hifdhi ya Qur'ani baada ya kulinganisha matokeo na kiraa za washindani.
Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Elimu ya mkoa wa Jericho Muhammad al Hawash alihutubia sherehe za kumalizika mashindano hayo ya Qur'ani akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwepo mashindano ya Qur'ani na masuala ya kidini hususan kwa watoto wadogo na katika kukuza vipawa vyao vya kuhifadhi Qur'ani.
Mwishoni washindi wa kwanza walitunukiwa zawadi kutoka kwa kamati iliyosimamia mahindano hayo. 716629