IQNA

OIC yataka jamii ya kimataifa ishughulikie kadhia ya Quds

12:56 - December 25, 2010
Habari ID: 2052691
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) amewaandikia barua Mawaziri wa Mambo ya Nje nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hatari zinazukabili Msikiti wa Al Aqsa kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Katika barua hiyo Katibu Mkuu wa OIC Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu amesema OIC inaitazama kadhia ya Msikiti wa Al Aqsa kuwa mstari mwekundu na kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel unaokalia kwa mabavu eneo hilo utabeba lawama za yoyote yatakayotokea dhidi ya usalama wake.
Katibu Mkuu wa OIC ametoa wito kwa Wanachama wa Kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzuia jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel ambazo ni pamoja na hujuma za mara kwa mara na kuruhusu mashirika ya wakfu ya Kiislamu kutekeleza kazi za ukarabati katika msikiti huo.
Katibu Mkuu wa OIC pia amemuandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO na kumtaka abuni kamati ya wataalamu wa kimataifa watakaoshirikiana na wataalamu wa wanachama wa OIC kwa lengo la kutathmini usalama wa Msikiti Mtakatifu wa Al Aqsa.

717635
captcha