IQNA

Arbaeen ya Imam Hussein (as) kufanyika London

12:47 - December 26, 2010
Habari ID: 2053278
Maombolezo ya Arbaeen ya Imam Hussein (as) maalumu kwa wanaozungumza lugha ya Kiingereza yamepangwa kufanyika tarehe 21 hadi Januari 24 mwakani huko katika mji wa London, Uingereza.
Maombolezo hayo ambayo yameandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha London yatakuwa yakifanyika kuanzia saa moja hadi tatu usiku kwa wakati wa Uingereza katika ukumbi wa maktaba kuu ya kituo hicho.
Kituo hicho cha Kiislamu pia kimeandaa maombolezo tofauti ambayo yatafanyika kwa lugha ya Kifarsi kwa wakazi wa London kwa mnasaba wa Arbaeen ya Imam Hussein (as), kifo cha Mtume (saw) na kuuawa shahidi maimamu Hassan Mujtaba na Ali bin Musa ar-Ridhaa (as) tokea tarehe 25 Januari.
Maombolezo hayo yatakayokuwa yakianza saa moja na nusu usiku yataendelea hadi tarehe 3 Februari. 717771
captcha