Kwa mujibu wa tovuti ya Zawya, sherehe hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya wataalamu 300 wa masuala ya uchumi wa Kiislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia kwa ajili ya kuchagua na kutoa shukrani kwa taasisi na mashirika ya kiuchumi ya Kiislamu. Taasisi 30 zilichaguliwa kuwa taasisi bora zaidi za kiuchumi na kibiashara katika ulimwengu wa Kiislamu.
Thuluthi moja ya zawadi zilizotolewa katika shehere hiyo iliwaendea wanabenki na wataalamu wa masuala ya kiuchumi na benki za Kiislamu za nchi za Ghuba ya Uajemi na zilizosalia zilichukuliwa na taasisi pamoja na mashirika ya kifedha ya Kiislamu yanayoendeshea shughuli zao katika nchi za Uingereza, Marekani, Malaysia, Luxembourg na Sudan. 718122