IQNA

Mahafidh na makarii wa Qur'ani Palestina waenziwa

16:46 - December 27, 2010
Habari ID: 2054221
Sherehe za kuwaenzi makarii na mahafidha wa Qur'ani Tukufu huko Palestina zimefanyika katika mji wa Ramallah.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe hizo zilifanyika Jumamosi alasiri 25 Disemba na kuhudhuriwa na Mahmoud Al-Habash Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Palestina, Leili Ghanam Mkuu wa Mkoa wa Ramallah na shakhsia wa ngazi za juu pamoja na Makarii na Mahafidh wa Qur'ani wa Palestina.
Mahmoud Al-Habash amesema Wizara ya Wakfu ya Palestina inatoa huduma kwa Qur'ani Tukufu mbali na kuchapisha majarida ya kiutamaduni. Ameongeza kuwa kutoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu kupitia misikiti, shule na vyuo vikuu ni kati ya masuala yanayopewa kipaumbele na wizara yake. 719139


captcha