Mtandao wa habari wa jumuiya ya IIDR umeripoti kuwa kikao hicho cha mafunzo kitakachosimamiwa na Akademia ya Utafiti wa Qur'ani ya Uingereza (BAQS) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha London, kitachunguza pande mbalimbali za suratul Hadid kama sababu ya kuteremshwa kwake, mafundisho yaliyomo, sisitizo la Mwenyezi Mungu katika sura hiyo kuhusu maisha ya kijamii, sifa makhsusi za jamii ya Kiislamu na udharura wa kutoa mali katika njia Mwenyezi Mungu.
Masuala mengine yatakayojadiliwa ni njia za kuimarisha imani na kumtegemea Mwenyezi Mungu na faida zake kwa wanadamu
Wasomi na maulamaa kadhaa wa Kiislamu wa Ulaya.
Akademia ya Utafiti wa Qur'ani ya Uingereza BAQS ni taasisi iliyochini ya Jumuiya ya Kiislamu ya Ustawi na Utafiti ya IIDR iliyoasisiwa kwa ajili ya kutoa elimu na kufanya utafiti wa masuala ya Qur'ani. Jumuiya hiyo inajishughulisha pia na kutoa mafunzo ya muda, semina za masuala ya Qur'ani, kutayarisha walimu wa kitabu hicho, kubuni ratiba na kuchapisha makala za uchunguzi kuhusu Qur'ani Tukufu.
Akademia hiyo hufanya kikao mara moja kika mwezi katika miji mbambali ya Uingereza. 718673