IQNA

Qur'ani ina nafasi muhimu katika umoja

12:58 - December 28, 2010
Habari ID: 2054442
Sheikh Saleh Bin Abdulaziz Al Sheikh Waziri wa Masuala ya Kiislamu nchini Saudi Arabia ameshiriki katika sherehe za kufungua Mashindano ya 32 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani mjini Makka na kusisitiza juu ya nafasi ya Qur'an katika Umoja wa Kiislamu.
Akizungumza katika sherehe za kufunga mashindano ya Qur'ani ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika katika Masjidul Haram, Al Sheikh amesema kuwa kuwa Qur'ani Tukufu ina nafasi katika kuimarisha umoja na mshikamano wa umma wa Kiislamu. Ameongeza kuwa hivi sasa kunafanyika juhudi za kusambaza ujumbe wa Qur'ani kote duniani.
Amesema kuwa kujifunza, kuhifadhi na kutekeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu katika sekta zote za maisha ni wajibu wa Waislamu wote na kuongeza kuwa, "Qur'ani ina nafasi muhimu sana katika maisha ya Waislamu na ustawi wa ustaarabu wa Kiislamu unatokana na baraka za kitabu hicho cha mbinguni'.
Mashindano ya 32 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani ya Malik Abdulazizi yamefanyika kwa himaya ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudia na yaliwakutanisha pamoja washiriki 188 kutoka nchi 54 duniani.
Mashindano hayo yana viwango vitano vya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa kuzingatia sheria za tajwidi pamoja na tafsiri. Washiriki watashindana katika kuhifadhi Qur'ani Kamili, Juzuu 20, Juzuu 10 na Juzuu 5.
Washindi wa kwanza watano katika kila kiwango watatunukiwa zawadi na washiriki wote watapata fursa ya kutekeleza ibada ya umra.
719345
captcha