IQNA

Mafunzo ya Qur'ani kutolewa Afrika Kusini

16:53 - December 28, 2010
Habari ID: 2055049
Mafunzo ya muda ya Qur'ani na maarifa ya kitabu hicho makhsusi kwa watoto wadogo yataanza kutolewa mwaka mpya wa 2011 katika Taasisi ya Utafiti wa Sheria za Kiislamu katika eneo la Heideveld katika mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini.
Taasisi ya Qur'ani ya Afrika Kusini imeripoti kuwa masomo hayo yatakuwa yakitolewa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kwa wanafunzi wa kike na kiume. Ripoti hiyo imesema kuwa watoto hao watapewa mafunzo ya Qur'ani na maarifa ya kitabu hicho.
Ripoti hiyo imesema kuwa watoto hao kwanza watafundishwa sheria za tajwidi, kiraa na mbinu za kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Vilevile watapewa mafunzo ya lugha ya Kiarabu kwa ajili ya kuelewa vyema Qur'ani Tukufu na elimu mbalimbali za Kiislamu.
Watoto wenye juu ya umri wa miaka mitatu watakaoshiriki katika masomo hayo wataweza kusoma Qur'ani Tukufu na kuhifadhi aya zake baada ya kukamilisha masomo hayo.
Masomo hayo ambayo yanafanyika kwa lengo la kuwafundisha watoto utambulisho wa Kiislamu yataendelea kwa kipindi cha mwaka mzima. 720036

captcha