Gazeti la Saudi gazette limeandika kuwa habari hiyo imetangazwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Kuhifadhi Qur'ani ya Makka Abdullah Umar Nasif ambaye ameongeza kuwa Amir wa Makka ameanzisha mfuko huo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo ya mara kadhaa na viongozi wa jumuiya hiyo.
Amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kufuatia uamuzi wa serikali ya Saudi Arabia ya kutumia walimu wa ndani katika vituo vya kufundishia Qur'ani.
Nasif amesema kuwa juhudi zimekuwa zikifanyika kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita kwa ajili ya kuajiri walimu wa Qur'ani wa taasisi na vituo vya kufundisha kitabu hicho lakini juhudi hizo hazikuwa na mafanikio kutokana na malipo duni yanayotolewa kwa walimu hao.
Kuhusu walimu wa Qur'ani wasiokuwa Wasaudia, Abdullah Umar Nasif amesema kuwa walimu hao wanaweza kuendelea na kazi zao iwapo watapasishwa na taasisi husika. 719969