IQNA

Sarawak ya Malaysia Yatumia Mifuko Rafiki kwa Mazingira Katika Hafla ya Utupaji wa Majivu ya Misahafu

12:08 - June 22, 2026
Habari ID: 3482388
IQNA – Jimbo la Sarawak nchini Malaysia limetekeleza zoezi la kuweka ndani ya bahari kilo 1,802 za majivu ya misahafu ya Qur’ani Tukufu katika Bahari ya China Kusini siku ya Jumamosi, kwa kutumia mifuko maalumu ya karatasi inayoweza kuzorota kirahisi bila kudhuru mazingira.

Majivu hayo yaliwekwa katika mifuko maalumu 212 ya karatasi rafiki kwa mazingira aina ya AQ‑01, yaliyotokana na mchakato kuhifadhi nakala za Qur’ani zilizoharibika katika vituo vya maalumu vya kuweka baharini maneneo hayo matukufu kote Sarawak.

Mkuu wa Kitengo cha Qur’ani katika Idara ya Masuala ya Kiislamu ya Sarawak (JAIS), Abdul Rahim Rashid, amesema kuwa zoezi hilo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida unaofanywa kwa mujibu wa uamuzi wa Muzakarah ya Kamati ya Kitaifa ya Fatwa, kwa lengo la kulinda heshima na utukufu wa maandishi ya Qur’ani Tukufu yaliyoharibika kulingana na hukumu za Sharia.

“Ama kwa hakika, huu ni mpango wa mara kwa mara wa kuachia majivu ya misahafu baharini, unaotekelezwa kufuatia maamuzi ya Muzakarah ya Kamati ya Kitaifa ya Fatwa, katika juhudi za kuhifadhi heshima ya nyenzo za Qur’ani Tukufu zilizopata uharibifu,” alisema alipokutana na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Kituo cha Feri cha Pending mjini Kuching.

Aliongeza kuwa kila mfuko una uzito wa takribani kilo 8.5 na umetengenezwa kwa namna ya kuzama haraka na kisha kuzorota kikamilifu ndani ya muda usiozidi dakika nne, jambo linalohakikisha kuwa zoezi la uwekaji baharini linafanyika kwa utaratibu, kwa heshima, na kwa namna rafiki kwa mazingira.

Hafla hiyo kubwa, ikiwa ni ya kwanza ya aina yake katika kusini mwa Sarawak, ilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mufti wa Sarawak Ahmad Sukarno Saini, Naibu Mkurugenzi wa Walinzi wa Pwani wa Sarawak Paul Khiu Khon Khiang, Mkuu wa Operesheni za Ujasusi wa Kikosi cha Polisi wa Majini Mkoa wa 5 Sarawak DSP Mohd Noor Mohd Yassin, pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Utekelezaji na Udhibiti katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Sarawak Asydidi Hamzah.

3497914

Kishikizo: qurani tukufu malaysia
captcha