Gazeti la Madina limelipoti kuwa Katibu wa mashindano hayo Mansour bin Muhammad al Samiih amesema washiriki 30 kutoka nchi tofauti walichuana jana katika vitengo tofauti vya kiraa, hifdhi na tafsiri ya Qur’ani.
Amesisitiza kuwa mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza ndani ya Masjidul Haram na kwamba lengo la hatua hiyo ni kujenga uhusiano mkubwa zaidi kati ya vijana na Kitabu Kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.
Mansour bin Muhammad al Samiih amesema kandokando ya mashindano hayo kunatolewa mafunzo ya majaji wa mashindano ya Qur’ani.
Mashindano ya Kimataifa ya 32 ya Qur’ani Tukufu ya Saudi Arabia yalianza Jumatatu iliyopita katika nyanja za hifdhi, kiraa na tafsiri ya Qur’ani Tukufu. Mashindano hayo yanayofanyika katika mji mtakatifu wa Makka yanarushwa hewani moja kwa moja kupitia Redio Qur’ani ya Saudia. 720613