IQNA

Mashindano ya Qur'ani kuwasilisha taswira halisi ya Iran

12:48 - December 30, 2010
Habari ID: 2055924
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yanaweza kuwa na mchango muhimu katika kuwasilisha taswira halisi ya Kiislamu ya Iran duniani.
Hayo yamesemwa na Issa Alizadeh Mkuu wa Jumuiya ya Shughuli za Qur'ani ya Wanachuo Wairani alipozungumza na IQNA. Ameongeza kuwa mashindano hayo pia ni fursa ya kielimu na kisayansi kwa wanachuo Waislamu.
Akifafanua kuhusu mashindano hayo ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yatakayofanyika Januari 9-12 2011 katika mji wa Mtakatifu wa Mash'had kaskazini-mashariki mwa Iran, amesema kuwa: "Fikra ya mashindano ya Qurani maalumu kwa wanafunzi Waislamu katika vyuo vikuu duniani ilibuniwa baada ya duru 20 za mashindano ya Qur'ani maalumu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iran yaliyoandaliwa na Shirika la Jihadi ya Vyuo Vikuu. Baada ya kuanzishwa Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa, wasimamizi wa sera katika Shirika la Jihadi ya Vyuo Vikuu waliamu kuanzisha mashindano ya Qur'ani katika kiwango cha kimataifa (ya wanafunzi wa vyuo vikuu) ili kuwapa motisha wanafunzi Wairani wafanye bidii zaidi katika sekta ya shughuli za Qur'ani" 720295

captcha