Gazeti la Arab News limeandika kuwa serikali ya Saudia imelazimika kufuta marufuku hiyo kutokana na uhaba wa walimu wa Qur'ani raia wa nchi hiyo na kutangaza kuwa walimu wa Qur'ani wasiokuwa Wasaudia wanaweza kuendelea na kazi zao katika vituo vya kufunza kitabu hicho iwapo watakuwa na sifa zinazohitajika.
Serikali ya Saudi Arabia imetaja masharti ya kuwa na cheti cha Qur'ani na kutokuwa na historia mbaya nchini kuwa ni masharti anayopaswa kuwa nayo raia wa kigeni anayefundisha Qur'ani katika vituo vya kufundisha kitabu icho.
Mkuu wa ofisi ya Jumuiya ya Kheri ya Kuhifadhisha Qur'ani Tukufu ya Saudi Arabia Abul Aziz bin Abdullah Hanafi amesema kuwa kwa sasa kuna shule 100 tu za kutoa mafunzo ya Qur'ani za raia wa nchi hiyo na kwamba idadi hiyo haikidhi mahitaji yaliyopo katika uwanja huo.
Amesema kuwa juhudi zimefanyika kwa ajili ya kuwahamasisha watu kujifunza na kufunza Qur'ani Tukufu lakini kutokana na uhaba wa walimu raia wa Saudi Arabia, serikali italazimika kuajiri walimu wa kigeni wa Qur'ani. 720930