IQNA

Mashindano ya kuhifadhi Hadithi za Mtume SAW yamalizika Madina

12:31 - January 01, 2011
Habari ID: 2056231
Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Hadithi za Mtume SAW makhsusi kwa wanafunzi wa shule za mji wa Madina yajulikanayo kama “Amri Anif bin Abdulaziz” yalimalizika Alhamisi Desemba 30.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yalikuwa utangulizi wa mashindano ya kimataifa ya Suna ya Mtume SAW makhsusi kwa wasomi wa Kiislamu ambayo yana anwani ya “Zawadi ya Naif bin Abdulazizi”.
Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Hadithi za Mtume SAW makhsusi kwa wanafunzi wa shule za mji wa Madina yalihudhuriwa na Mkuu wa Masuala ya Elimu mjini humo.
Lengo la mashindano hayo ya kiutamaduni limetajwa kuwa ni kustawisha akhlaqi na maadili mema ya vijana na kuwapa motisha wa kuchukua kigezo katika sira ya Mtume SAW.
Baada ya kumalizika mashindano hayo, wanafunzi sita bora wametunukiwa zawadi. 721523
captcha