IQNA

Mwanasiasa Mholanzi kuchapisha kitabu kilichodhidi ya Uislamu

16:50 - January 01, 2011
Habari ID: 2056828
Mwakilishi mwenye misimamo ya kufurutu mipaka wa bunge la Uholanz Geert Wilders ambaye ndiye aliyetengeneza filamu ya Fitna inayokivunjia heshima kitabu kitukufu cha Qur'ani amesema kuwa atachapicha kitabu kinachohujumu dini ya Kiislamu katika mwaka huu mpya wa 2011.
Kituo cha habari cha gnet cha Tunisia kimeripoti kuwa Wilders ameliambia gazeti la Telegraph la Uholanzi kwamba lengo la kuchapicha kitabu hicho na kukitawanya kwa wingi katika masoko ya vitabu ya Marekani na kupanua zaidi mapambano ya kimataifa dhidi ya Uislamu.
Kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha Uhuru cha Uholanzi amenukuliwa akisema katika matamshi yake hayo ya dharau na kiburi kwamba: "Nchini Uholanzi tunaweza kufanya kazi nyingi kwa ajili ya kupambana na Uislamu na tuna nia ya kudhihirisha taathira za kazi hii katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu; kwa msingi huo tunafanya juhudi za kueneza zaidi mapambano haya katika uga wa kimataifa."
Mwanasiasa huyu mwenye chuki na uhasama dhidi ya Uislamu wa Uholanzi amesema kitabu hicho kitachapishwa mwaka huu wa 2011 na kitafafanua njia za kukabiliana na Uislamu katika medani za kimataifa. 721856
captcha