IQNA

Kongamano la Uislamu na Vyombo vya Habari kufanyika Uturuki

13:16 - January 03, 2011
Habari ID: 2057895
Kongamano la Uislamu na Vyombo vya Habari limepangwa kufanyika mjini Istanbul Uturuki tokea tarehe 13 hadi 17 Julai mwaka huu kwa lengo la kujadili matukio mapya katika vyombo vya habari na magazeti katika ulimwengu wa Kiislamu.
Kongamano hilo ambalo litawajumuisha wanafikra na wasomi wa Kiislamu katika uwanja wa vyombo vya habari kutoka kote ulimwenguni limepangwa kufanyika katika Chuo Kikuu cha Kadir Has na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Vyombo vya Habari na Mawasiliano IAMCR.
Kongamano hilo la siku tano litajadili masuala mbalimbali yakiwemo ya Uislamu; mawasiliano na mazungumzo ya tamaduni, Uislamu; zama za dijitali na uvumbuzi, Uislamu; uhai mpya na uraia, sura ya Uislamu na Waislamu katika vyombo vya habari vya kimataifa, sura ya wasio Waislamu katika vyombo vya habari vya Kiislamu, vyombo vya habari vya kijamii na uvumbuzi wa vijana wa Kiislamu, usanii na utamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu na Ulaya na Uislamu; nafasi ya vyombo vya habari. 722869
captcha