Kwa mujibu wa tovuti ya APA madrasa hiyo ya Qur'ani inajumuisha sehemu ya kuswalia, kituo cha Kiislamu, madarasa maalumu ya kufundishia hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu na ukumbi wa mikutano.
Akizungumzia suala hilo mbele ya waandishi habari, Muhammad Lamin Baji, Balozi wa Gambia nchini Mauritania amesema kuwa madrasa hiyo pia inaweza kutumiwa na Wagambia wanaoishi nchini Mauritania kama kituo cha kutafuta elimu na hasa elimu inayohusiana na masomo ya Kiislamu.
Amesema katika sehemu nyingine ya hotuba yake kwamba misikiti ya Mauritania inatumiwa kama vituo muhimu vya kupata masomo na thamani nyinginezo za Kiislamu na Qur'ani bila ubaguzi wowote wa kitaifa.
Kituo hicho cha Qur'ani kilifunguliwa siku ya Ijumaa tarehe 31 Disemba mwaka uliopita ambapo balozi huyo na viongozi wa serikali ya Mauritania walihudhuria. 724161