IQNA

Utawala wa Kizayuni ulitumia tani 3000 za mada za milipuko katika mashambulio yake Gaza

11:39 - January 06, 2011
Habari ID: 2059839
Polisi ya Ukanda wa Gaza imetangaza kwamba katika mashambulio yake ya kinyama ya siku 22 katika ukanda huo, utawala ghasibu wa Israel ulitumia tani 3000 za mada za milipuko yakiwemo mabomu, makombora, mizinga na risasi.
Akibainisha suala hilo, Tahsin Sad, mkuu wa kitengo cha uhandisi wa mada za milipuko cha polisi ya Gaza amesema kuwa, mingi ya milipuko hiyo imepigwa marufuku na sheria za kimataifa. Sad amesema katika taarifa kwamba utawala wa Kizayuni ulitumia milipuko hiyo kama sehemu ya kufanyia majaribio baadhi ya silaha zake ilizorundika kwenye maghala ya silaha.
Ameshangazwa na ukweli kwamba licha ya kuwa utawala huo ulifanya jinai hiyo dhidi ya Wapalestina lakini waitifaki wake ikiwemo Marekani na nchi za Ulaya wamefunga mikataba mipya ya kuuuzia utawala huo silaha za kisasa. Amesema silaha hizo hazijakuwa na athari za moja kwa moja za kuwaangamiza wananchi wasio na hatia wa Palestina tu bali zimekuwa na athari yingine za muda mrefu ikiwa ni pamoja na kulemaza watoto wanaozaliwa na kuwaambukiza waathirika wengi maradhi hatari ya kansa.
Polisi ya Gaza hivi sasa inakusanya silaha na mabomu ambayo hayakulipuka wakati wa hujuma hiyo ya Israel kwa lengo la kuushtaki mahakamani utawala huo. 725029
captcha