IQNA

Wabahraini 15,000 kufanya ziara Karbala siku ya Arbaini ya Imam Hussein (as)

13:34 - January 08, 2011
Habari ID: 2060458
Wabahraini wapatao 15,000 wanatazamiwa kuelekea Karbala katika siku chache zijazo kwa madhumuni ya kushiriki kwenye maombolezo ya Arbaini ya Imam Hussein (as).
Akizungumzia suala hilo Swalah al-Maliki, balozi wa Bahrain nchini Iraq amesema kuwa ubalozi huo pamoja na ubalozi mdogo wa Bahrain katika mji mtakatifu wa Najaf ziko tayari kukaribisha na kuwahudumia Wabahraini ambao wanatazamiwa kuanza safari hiyo katika kipindi cha wiki mbili zijazo. Amesema kuwa ubalozi huo umeanzisha ofisi nyingine ya muda katika hoteli ya Jarsh huko Karbala kwa madhumuni ya kuwahudumia wafanyaziara wa nchi hiyo wanaotazimiwa kufanya safari katika mji huo katika siku za hivi karibuni.
Amin al-Madhub mmoja wa wakurugenzi wanaosimamia safari za Wabahraini nchini Iraq amesema kuwa raia hao wanatazamiwa kuingia nchini Iraq kupitia viwanja vya ndege vya Bagdad, Najaf na vilevile kupitia mipaka ya nchi kavu ya Kuwait na Syria.
Mwaka uliopita Wabahrain wapatao 24,000 walifanya ziara nchini Iraq kwa ajili ya kushiriki katika maombolezo ya Arbaini ya Imam Hussein (as).
Kwa mujibu wa takwimu zlizotolewa na maafisa husika, 13,000 kati ya wasafiri hao walikuwa ni Washia wa Saudi Arabia ambao waliingia Iraq kutokea Bahrain. 725768
captcha