Mbali na kushiriki katika kongamano hilo litakalofanyika katika jimbo la Kerala, Mufti Ali Gomaa atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu wa serikali akiwemo Makamu wa Rais wa nchi hiyo Hamid Ansari.
Balozi wa Misri nchini India Khaled al-Baqly amesema Sheikh Gomaa atahutubia mkutano huo utakaohudhuriwa na wasomi na maulamaa kutoka maeneo mbalimbali duniani. Amesema Mufti Gomaa atazungumzia kuhusu ujumbe wa Uislamu kwa walimwengu na jinsi ya kuishi kwa amani wafuasi wa dini na tamaduni tofauti.
Baadhi ya viongozi wa kisiasa wa nchi za Kiislamu na viongozi wa madhehebu za Kiislamu watashiriki katika kongamano hilo la kimataifa. 726978