Maudhui za kitabu hicho zinajumuisha uchunguzi kuhusu itikadi ya kuwepo Imam Mahdi (as), kuzaliwa na maisha yake, kwenda kwake ghaiba ndogo, ghaiba kubwa, hali ya wakati wa kudhihiri kwake, wafuasi wake kwa mujibu wa itikadi na mafundisho ya Ahlul Bait (as) na kadhalika.
Mwandishi wa kitabu hicho amekusanya maudhui kuhusu kuzaliwa kwa Imam Mahdi (as), kughibu na kudhihiri kwake kutoka katika vitabu vya Kisuni.
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait imeamua kuchapicha tena kitabu hicho kwa mara ya tatu kutokana na umuhimu wa maudhui zake. 727387