IQNA

Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa Bidhaa Halali kufanyika Kuwait

18:47 - January 10, 2011
Habari ID: 2062282
Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa Bidhaa Halali katika Mashariki ya Kati utafanyika tarehe 24 hadi 26 Januari katika mji wa al Salimiyya nchini Kuwait.
Tovuti ya Halal Focas kimeripoti kuwa mkutano huo wa siku tatu utasimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait, Tasisi ya Uhakiki wa Sayansi ya Kuwait, Shirika la Viwango la Mashariki ya Kati na jumuiya nyingine kadhaa.
Lengo la mkutano huo limetajwa kuwa ni kutayarisha ripoti sahihi na za hivi karibuni kuhusu sekta na huduma ya bidhaa halali, kuchunguza uhalali wa bidhaa zinazopatika katika masoko, kuchinja wanyama kwa kutumia ala za elektroniki, kuwatambulisha washiriki kuhusu masuala ya kiufundi na kiuchumi ya sekta ya bidhaa halali na huduma zake na kuchunguza suala la kuanzishwa viwango vya kimataifa vya bidhaa halali.
Masuala mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na mada za kemikali zinazotumiwa katika vyakula, mada zinazotumiwa katika bidhaa za urembo na mapambo na kadhalika.
Makala za mkutano huo zitawasilishwa kwa lugha mbili za Kiingereza na Kiarabu. 727828



captcha