IQNA

Kongamano la Waislamu Wapya lafanyika The Hague, Uholanzi

18:48 - January 10, 2011
Habari ID: 2062285
Taasisi ya Kashful Islam imeitisha kongamano la watu walioingia katika dini tukufu ya Kiislamu katika mji wa Hague nchini Uholanzi.
Gazeti la Kuwait Times limeripoti kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Kitaifa ya Waislamu Wapya ya Uholanzi Walid Duwaisters amesema katika kongamano hilo kwamba vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vinafanya njama za kuonyesha taswira mbaya kuhusu Waislamu wapya. Amesema kuwa kongamano hilo linakusudia kuonyesha taswira halisi ya Waislamu wapya.
Duwaisters ameongeza kuwa takwimu zilizotolewa mwaka 2007 zinasema kuwa katika miaka ya hivi karibuni Waholanzi 12000 hadi 14000 wameingia katika dini ya Kiislamu na kwa kutilia maanani kwamba watu wote wanaoingia katika dini ya Kiislamu hawatangazi rasmi mabadiliko hayo, hapana shaka kwamba idadi hiyo ni kubwa zaidi kuliko iliyotangazwa rasmi.
Uholanzi ina jamii ya karibu watu milioni 17 na karibu milioni moja kati yao ni Waislamu. 727880

captcha