IQNA

Wito wa kuimarisha mfumo wa hisa za benki za Kiislamu

13:08 - January 15, 2011
Habari ID: 2064594
Gavana wa Benki Kuu ya Lebanon Riad Salamah ametoa wito wa kuimarishwa hisa za mashirika ya Kiislamu.
"Huku masoko ya Kiislamu ya hisa yakizidi kuimarika, yatavutia wawekezaji wa kimataifa wanaotaka faida na fursa zaidi", amesema Salamah.
"Vigezo vya Kiislamu vitakuwepo kuwasaidia wawekezaji na kuongeza uwezo wa uwekezaji zaidi katika masoko ya Kiislamu", ameongeza Salamah.
Salamah amesema kutokana na kutokuwepo mfumo wa kifedha wa Kiislamu hadi mwaka 1987, aghalabu ya wawekezaji Waislamu hawakuingia katika masoko ya hisa.
Hata hivyo amesisitiza kuwa benki za Kiislamu hazijastawi ipasavyo nchini Lebanon pamoja na kuwa zimekuwepo nchini humo kwa miaka minane sasa.
730153
captcha