Kikao hicho kitajadili masuala muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu ikiwa ni pamoja na hali ya Wakristo katika jamii za Kiislamu na jinsi ya kudhamini haki zao za kiraia na kisiasa na pia juhudi za kuzuia njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kutaka kuyahudisha Quds Tukufu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Sekretarieti ya Baraza la Taifa la Federesheni ya Imarati imetangaza kuwa hadi sasa maspika na ujumbe za mabunge ya zaidi ya nchi 50 za Kiislamu zimewasili Imarati na kwamba kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Federesheni ya Imarati Abdul Aziz Abdul Aziz.
Vilevile kikao cha pili cha dharura cha Umoja wa Mabunge ya Kiislamu kitafanyika Jumatano ijayo na kuchunguza changamoto za kieneo na kimataifa zinazokabili mwamko na usalama wa ulimwengu wa Kiislamu, suala la kulinda Quds Tukufu, matumizi ya nishati ya nyuklia kwa malengo ya kiraia katika nchi za Kiislamu na mazungumzo na ushirikiano na mabunge ya nchi za Magharibi. 730496