Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO na Wizara ya Masuala ya Dini ya Senegal zimejadili jinsi ya kuitisha mkutano wa wasomi wa Kiislamu katika mji mkuu wa nchi hiyo Dakar.
Katibu Mkuu wa ISESCO Abdul Aziz Othman al Tuweijri na Waziri wa Masuala ya Dini wa Senegal Mamadou Bamba wamekutana na kujadili jinsi ya kuitisha mkutano huo utakaosimamiwa na pande hizo mbili.
Siku chache zilizopita pia kulifanyika kikao cha awali cha matayarisho ya mkutano wa wasomi wa Kiislamu ambao ulihudhuriwa na Rais Abdoulaye Wade wa Senegal Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamau OIC. Kikao hicho kilichunguza masuala na matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu na wakati na mahala mkutano wa wasomi wa Kiislamu utakapofanyika.
Imepangwa kuwa mkutano huo utaanza tarehe 1 Mchi mwaka huu. 730464