Kwa mujibu wa gazeti la Al Sharq linalochapishwa Qatar, mashindano hayo yatawashirikisha vijana wa kike na kiume kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu.
Kamati ya kuandaa mashindano hayo imesema nukta zitakazozingatiwa ni pamoja na sheria za tajwid na umaridadi wa sauti na lahni na kila mshiriki atapewa dakika tatu kuonyesha ustadi wake katika kiraa.
Wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanapaswa kujiandikisha kabla ya tarehe tano Februari katika tovuti ya Islamweb.
Jopo la majaji katika mashindano hayo linajumuisha maulamaa na wataalamu wa Qur'ani Tukufu.
732068