IQNA

Masomo ya muda ya tafsiri ya Qur’ani kuanzishwa Dallas

17:38 - January 18, 2011
Habari ID: 2066951
Taasisi ya elimu ya Bayyinah imeazimia kuanzisha masomo ya muda ya tafsiri ya Qur’ani katika mji wa Dallas nchini Marekani katika kipindi cha kiangazi mwaka huu.
Kituo cha Bayyinah.com kimeripoti kuwa mbali na tafsiri ya Qur’ani, masomo hayo pia yatajumuisha lugha ya Kiarabu.
Baadhi ya maudhui zitakazojadiliwa katika darsa hizo za tafsiri ya Qur'ani ni pamoja na fasihi ya Qur'ani, tafsiri kwa mujibu hadithi, Suna za Mtume na tafsiri ya Qur'ani na uchambuzi wa isimu ya Qur'ani.
Masomo hayo ya muda yataendelea kwa kipindi cha siku 30 kwa shabaha ya kueneza ujumbe wa Qur'ani Tukufu na utambuzi bora zaidi wa mafundisho yake.
Taasisi ya Bayyinah iliasisiwa nchini Marekani kwa nia ya kueneza lugha ya Kiarabu katika miji mbalimbali ya nchi hiyo. 732758
captcha